Published on 13/03/2025 by Dayo Radio
Kila baada ya muda Raisi huwa na Ziara katika Taifa letu la Kenya Ziara ya hivi punde ikiwa ni Eneo la Pwani ambapo

Takriban wiki nzima Raisi ametembelea sehemu nyingi za pwani kufungua miradi inayolenga kumfaidi mwananchi na hasa mkazi wa pwani.
Miradi ilio tia fora zaidi ni ile ya uzinduzi wa Nyumba za Bei nafuu.Takriban kila Kaunti ya Pwani iliweza kupata ya kupata kuanzishwa kwa jiwe la msingi kwa Minajili ya kuanza Rasmi kwa ujenzi huo.
Vijana wenye Walisomea kazi tofauti tofauti Wanaweza kupata Fursa kujiunga katika Nyumba hizi na kupata vibarua
Mradi wa kuunganisha umeme katika sehemu ambazo hazijafikiwa na nguvu hizo za umeme pia ulinoga katika ziara ya Raisi Ruto ambapo yatakua manufaa makubwa kwa wakaazi wa pwani kujiendeleza kwa shughuli nyingi ndiposa viongozi na wananchi kutoka pwani walimpongeza Raisi Ruto kwa hatua hii ya kuunganisha umeme

Kilio cha Mpwani kuweza kupata hati miliki za mashamba pia kilionekana kupata jawabu kwa maana Raisi aliweza kutoa Hati miliki za kutosha kwa wenyeji huku wengine wakia hakikishiwa kua watakua wanatatuliwa shida hio kubwa iliokua ikiwazonga kwa siku nyingi
Swala la uzinduzi wa barabara pia halikuachwa Nyuma ziko nyingi ambazo ziliweza kuzinduliwa kwa manufaa ya mpwani aweze kujiendeleza kibiashara na kimaisha kiujumla hivyo ni Sharti kila mmoja aweze kulikumbatia hili.

Miongoni mwa miradi mingitu ambayo iliweza kuanzishwa ,swali ni je miradi hii itaendelezwa kadri vile Rais alivyo wahakikishia wapwani? au waliopewa kipao mbele katika miradi hii Watazifuja Mali za uma bila kujali?
Kwa mara nyingi tumeona miradi mingi ikizinduliwa ila baadae pesa hupotea katika mifuko ya watu kidogo hii hujma kwa wananchi wote.
Ni jukumu sasa kila mmoja kuweza kulinda ushuru wake sasa na endapo utapata fununu kwamba Mradi unaufujaji wa pesa na rasilimali za uma paza sauti na hatua hii itatusongesha mbele kimaendeleo.Ni jukumu pia kwa serikali husika kufatilia kwa ukaribu miradi hii muhimu ili kuhakikisha kua inatekelezwa ipasavyo na Wananchi pia ni jukumu letu sote kuweza tuepuke ufisadi na kuukemea endapo tutauona ukifanyika.