Ukosefu wa elimu kuhusu haki za afya ya uzazi miongoni mwa wanawake na wasichana, hasa kuhusu hedhi, upangaji wa uzazi, uavyaji mimba salama, na unyanyasaji wa kijinsia vimekuwa donda sugu humu nchini.
Viwango vya kuongezeka kwa mimba zisizotarajiwa, uavyaji mimba usio salama, na uwezo mdogo wa kupata huduma muhimu kutokana na unyanyapaa wa kitamaduni, vikwazo vya kijiografia vya upatikanaji wa huduma za afya, na vikwazo vya kijiografia kwa vijana ni muongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake.
Wanawake na wasichana wengi hawana uelewa wa kimsingi wa haki zao za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na kupata taarifa kuhusu hedhi, njia za kufnya uzazi wa mpango, na mbinu salama za kuavya mimba, na hivyo kuzuia kufanya maamuzi sahihi.
Vizuizi vya kijamii na kitamaduni, kanuni za kijamii na unyanyapaa unaozunguka miongoni mwa vijana, huzuia mijadala ya wazi kuhusu elimu ya afya ya uzazi na hivyo kusababisha upatikanaji mdogo wa taarifa na huduma.
Kutofikia vituo vya afya kwa urahisi kumechangia pakubwa wanawake wengi kutopata tiba na elimu inayofaa haswa katika maeneo ya vijijini, huzuia ufikiaji wa huduma bora za afya ya uzazi haswa kwa vijana ambao wanakabiliwa kukabiliwa na unyanyapaa kutokana na ufahamu wa elimu ya afya ya uzazi.
Ongezeko la swala hili kwa wanawake na vijana umetokana na kwamba
vituo vingi vya afya havina mazingira yanaweza kuwasaidia vijana na wale wanaotoa huduma za afya kwani wengine wa wahudumu wanakosa hata ujuzi ambao wanaweza kutumia kushughulikia mahitaji ya afya ya uzazi kwa vijana na kwa ufanisi.
Vizuizi vya ukusanyaji wa data ni moja ya changamoto katika kukusanya data kwa usahihi kuhusu masuala ya afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na kutoripoti mada nyeti kama vile uavyaji mimba na unyanyasaji wa kingono, zinaweza kusababisha takwimu zisizo sahihi.
Vikwazo vya sera na kisheria na mapungufu katika sheria kuhusu upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na kutoa mimba, inaweza kupunguza zaidi uwezo wa wanawake kutekeleza haki zao za uzazi.
Hata hivyo matokeo ya changamoto hizi hufanya
viwango vya mimba zisizotarajiwa kuongezeka na hata utoaji wa mimba usio salama kupanda zaidi na kumpelekea mhusika katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na ndoa za utotoni.
Fikra potofu kwa elimu ya wanawake kuhusu afya ya uzazi na fursa za kiuchumi zinaweza kuondolewa iwapo kutapatikana suluhu mwafaka.
Utekelezaji wa programu za elimu ya ngono inayolingana na umri katika shule ili kuongeza ufahamu na maarifa kuhusu afya ya uzazi na hata huduma za afya kwa wanawake na hata vijana.
Kuanzisha kliniki maalum zinazofaa kwa vijana na watoa huduma za afya waliofunzwa ushirikiano wa jamii itasaidia pakukubwa kuongeza ufahamu kuhusu masuala ya afya ya uzazi kupitia programu za kufikia jamii.
Katika upande mwengine ni lazima kuwe na marekebisho ya sera ya
kuimarisha sheria ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba salama
Uboreshaji wa ukusanyaji wa data na kuimarisha mbinu za kukusanya data ili kunasa kwa usahihi mahitaji na changamoto za afya ya uzazi.
NA HARRISON KAZUNGU