Kupanga uzazi
Featured Stories
Published on 11/11/2024

Kupanga uzazi ni moja wapo ya njia muhimu ya  kuyamudu maisha , japo  mara nyingi jamii huwa na tashwishi kuhusu Swala hili.

wapo wengi wanaodhani Kuwa mpango wa uzazi  kuwa husababisha  maradhi au kudhoofisha afya ya mtu, ila zote kasumba. ukweli nikwamba hakuna utafiti unaothibitisha moja Kwa moja Kwamba  mpango wa uzazi husababisha  maradhi au  huzorotesha afya bali inategemea na namna gani utakavyojitunza.

Kupanga uzazi kuna faida si haba, hutoa fursa Kwa Watoto  kuzaliwa Kwa mpangilio na pia  kuwapa nafasi ya kukua vyema na kufurahia malezi bora

kisayansi Mtoto mdogo anapozaliwa mwenzake hukosa amani na fuaha na hata afya yake mara nyingi huanza  kudhoofika

Mbali na hayo kupanga uzazi Vile vile hutoa fursa Kwa watoto kupata  nafasi ya kusoma , lakin endapo watoto watakuwa katika familia ni ngumu kukidhi mahitaji yao wote hali inayopelekea baadhi ya watoto kukosa elimu bora au kufikia viwango vya juu katika ELIMU Yao.

Aidha faida nyengine ya kupanga uzazi ni KWAMBA  humpatia mwanamke nafasi ya kupumzika hivyo kumuwezesha hupata afya bora na kunawiri zaidi.mwanamke anaezaa mara kwa mara afya yake ni tofauti na mwanamke anaezaa kwa mpangilio.

Licha yakwamba kuna kasumba Kuwa ,mwanamke anapopanga uzazi basi uchungu wakujifungua huongezeka zaidi ,wengine husema kuwa inamfanya mwanamke apate shida nyingi zaidi pindi anapobeba ujauzito.

wengine hukosa kupata damu zao za mwezi ,au hata wanapozipata huwa na uchungu usio wa kawaida.

"Nishawahi kudunga sindano ya miezi mitatu lakin nilipata tabu sana kiasi cha kuwa ninapopata hedhi ni uchungu kama nataka kuzaa , vile vile nilipata damu nyingi sana na nikiacha kutumia mfumo huu wakupanga uzazi"

utafiti zaidi unaonyesha kwamba , njia za kupanga uzazi hutofautiana na pia hulingana na nguvu za mwenye kutumia.. kupata matatizo kama yakuruka kwa hedhi, kuumwa na kichwa na kuhisi kisunzi, ni madhara ya muda tu ambao hupungua au hata kupotea baada ya miezi kadhaa.

Lakin je, unajua kwamba asilimia kubwa ya vijana hukosa kupata huduma za kupanga uzazi au afya ya uzazi.

 

 

Utafiti unaonyesha kwamba vijana ambao bado hawajaolewa mara nyingi hupata changamoto zakupata huduma hizi..mara nyingi wanaopofika katika vituo vya afya ,husimangwa au hata kunyimwa bidhaa hizi muhumu hali inayowapelekea kupata maradhi au hata mimba za mapema.

Kuna baadhi ya watoto ambao wapo chini ya umri wa miaka 18 lakin wanafanya ngono kiholela na hata wanapojaribu kutafuta huduma za kupanga uzazi,kwao huwa changamoto kupata huduma hizi. watoto wanapokua na ari au hamu ya kufanya mapenzi ni ngumu sana kuwakataza kutofanya tendo hilo bali wanafaa kupatia nasaha nahata kuwasaidia kujinga na kupata maradhi ,mimba na madhara mengineo.

Ikubukwe ya kwamba karne ya 21 , inachangamoto nyingi sana, watoto wanachepuka wakiwa katika umri mdogo sana na wanajua mengi kuliko wazazi wao na hii ni kutokana na utandawazi ulioshamiri ulimwenguni. Kuwanyima kupata huduma za afya ya uzazi ni sawa sawa na kusuka kamba ilihali shina lake linachomeka ,

 Tukianchana na hayo,kuna baadhi ya vitongoji au visiwa ambako hakuna  njia ya kupata huduma hizi kabisa, utafiti unaonyesha kwamba vijiji vingi vilivyoko kaunti ya kwale ,hakuna  vituo vya afya vinavyopeana huduma hizi.na hata kuliko na huduma hizo , bado si huduma rafiki kwa vijana,  hawapati huduma hizo inavyostahili, hali inayopelekea wengi wao kuwa wazazi wakiwa katika umri mdogo.

" mimi ni mkaazi wa kinango miaka 19, kwa kweli huku kwetu sioni kama kuna mashirika ambayo yanajihusisha na mambo haya ya afya ya uzazi na kama wapo basi hayafanyi kazi vilivyo sababu sijui chochote kuhusu kupanga uzazi."

"Mkaazi wa kijiji cha funzi ,hapa kisiwani kwetu ata hospital ni shida,  kuna zahanati pekee ambayo haijishuhulishi kabisa na mambo ya kupanga uzazi, hakuana ata  duka la dawa kama waeza nunua mpira yaani condom "

"Tunaomba serikali ifanye hima katika kutuletea huduma hizi vijijini haswa kaunti ya kwale"

Kuna umuhimu wa vitengo vya afya Kwa ushirikiano  na mashirika kufika nyanjani ili kupeana mafunzo ya afya ya uzazi,na kwa serikali pia izingatie namna yakukidhi mahitaji ya wanachi haswa kwenye vijiji ambako hakuna hospital kubwa ili tuweze kupunguza maafa yanayoshudiwa

Na kimtazamo wa mambo yalivyo , kuna haja yakufanya marekebisho kuhusiana na umri gani wa watoto wanafaa kupatia huduma za afya ya uzazi, sababu yakwamba watoto wengi wanashiriki mapenzi kabla yakufika umri wa miaka 18.

Yote Tisa kumi ni Kwa serikali ya kitaifa na zile za kaunti kupitia WIZARA ya afya KUSHIRIKIANA pamoja Ili kuendesha uhamasisho WA kutosha Kwa watu WA jinsia zote kuhusu umuhimu WA kupanga. Kufanya hivi hakutachangia tu  kuzaliwa Kwa Watoto wenye afya nzuri Bali pia kutoa fursa serikali kupanga mipango endelevu Kwa wananchi wake.

Photo courtesy 

 

Kenya family planning 2030

Hafsa Juma

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online