WIMBI LA UTEKAJI NYARA
Featured Stories
Published on 10/01/2025

Visa vya utekaji nyara vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Kenya vimeacha taifa likiwa na majonzi na hofu, hasa miongoni mwa vijana wanaojaribu kupaza sauti dhidi ya maovu na ukandamizaji.

wasemao husema kuwa hofu haina kinga , kwa kweli wanachi wamejawa na hofu na maswali kadha wa kadhaa swali kuu ni: Je, ni nani anayehusika na vitendo hivi, na kwa nini vijana hasa wamekuwa shabaha kuu?

Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR), watu 82 waliripotiwa kutekwa nyara kati ya Juni na Desemba mwaka 2024. Uchambuzi unaonyesha kwamba maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z, yaliyofanyika kati ya Juni na Julai kupinga Mswada wa Fedha, yalichochea mwelekeo huu wa utekaji.

Ikumbukwe kuwa "Upepo wa kisulisuli huvuna vimbunga" Hii ni.baada ya , hatua za kulinda waandamanaji zilibaki dhaifu, na badala yake, vijana waligeuka kuwa waathiriwa wa ukandamizaji wa kisiasa.

Katiba ya Kenya ya 2010 inalinda uhuru wa kila mtu. Kifungu cha 29 kinahakikisha haki ya uhuru na usalama wa mtu, kikiharamisha mtu kuwekwa kizuizini bila mashtaka au kutendewa unyama. Aidha, Kifungu cha 49 kinaweka wazi haki za watu waliokamatwa, kama kufahamishwa sababu za kukamatwa na kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24.

Swali kubwa linabaki: Je, haki hizi zinatekelezwa?
Au ni sheria imekua pambo na sikimbilio la haki tena

Matukio ya Ian Reses, ambaye alitekwa Desemba 2024 na mwili wake kupatikana barabarani, na ndugu Jamil na Aslam Longton waliopitia mateso mikononi mwa watekaji, ni baadhi ya mifano ya ukatili huu. Waathiriwa wengi waliorudishwa wakiwa hai, kama Billy Mwingi na Peter Muteti, wanakabiliana na matatizo makubwa ya kiakili na kimwili kutokana na mateso.

licha yakua  "Akili ni mali, lakini mateso huharibu mali", Wasemao husema kwamba vijana ndio taifa la kesho, Je mustakabali WA taifa hili utakuwa wa namna gani iwapo vijana wataendelea kufanyiwa ukatili wanapopaza sauti zao kuyapinga maovu ?

Swala hili limechukua mkondo wa kisiasa, huku baadhi ya viongozi wakitupiana lawama. Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ametuhumiwa kupanga visa hivi ili kuchafua serikali ya Kenya Kwanza, naye akijibu kwamba serikali yenyewe ndiyo inayohusika.

Serikali inapaswa kutekeleza kwa makini vifungu vya Katiba ya 2010, hasa Kifungu cha 29 na 49, kuhakikisha kwamba kila raia analindwa dhidi ya ukiukwaji wa haki zake za msingi.

Aidha Tume Huru ya Uchunguzi inafaa Kuunda tume huru ya kuchunguza visa vya utekaji nyara na kuwawajibisha wahusika bila kujali nafasi zao serikalini au kisiasa.

 

Mashirika ya kiraia, makanisa, na jamii ya kimataifa yanapaswa kushirikiana kulishinikiza serikali kuhakikisha haki inatendeka kwa waathiriwa wa visa hivi.

Bila kusahau kwamba Vijana wanapaswa kupewa nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya kitaifa na sera zinazowahusu.Serikali inajukumu la kulinda maisha ya Kila mkenya kama ilivyoainishwa katika katiba ya mwaka 2010 .


Visa vya utekaji nyara vinatishia taswira ya Kenya kama taifa lenye demokrasia na heshima za haki za binadamu. Serikali inapaswa kuchukua hatua thabiti kuhakikisha kuwa kila raia analindwa. Huu ni wakati wa kuchukua hatua za dharura ili kurejesha usalama na haki kwa vijana wa Kenya.

Vijana ni taifa la kesho, na bila haki kwao, taifa halina mwelekeo thabiti.

 

HAFSA JUMA

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online