Katika miaka ya hivi karibuni, visa vya mauaji ya kiholela na utupaji wa watoto wachanga vimeongezeka kwa kiwango cha kutisha. watoto wachanga wengi wameendelea kutupwa jaani au kuachwa bila msaada, hali inayoonyesha changamoto kubwa katika jamii.vile vile baadhi ya wanawake wanauliwa kisha kukatwa katwa na kutupwa majaani huku baadi yao zikiwa sehemu kadhaa za mwili hazipo.
Nini huenda ikawa chanzo cha uovu huu?
Aidha ni Ukosefu wa Elimu ya Afya ya Uzazi ambapo Vijana wengi hukosa elimu sahihi kuhusu uzazi wa mpango, hali inayopelekea mimba zisizotarajiwa na hatimaye utupaji wa watoto, au iwe ni
Umaskini na Ukosefu wa Usaidizi wa Kijamii pia huenda ikawa chanzo ambapo Wazazi wengi walio katika hali ngumu ya maisha huona watoto kama mzigo mkubwa kwenye maisha na baadhi yao huchukua maamuzi mabaya ya kuwatupa au kuwaangamiza watoto .
Katika karne hii bado wanaume hukata kata wake zao au kuwaua kwa kisingizio cha ugumu wa maisha .
Je ukosefu wa pesa au changamoto za maisha inafaa kuwa sababu za kumtoa uhai mke wako?
Katika siku za hivi karibuni , mwanamume mmoja jijini Nairobi alimua mke wake kisha baadae kumkatakata na kumueka kwenye gunia na katika kaunti ya mombasa eneo bunge la likoni. Kisa sawa na hicho kilishuhudiwa ambapo mwanamke mmoja alipatikana ametupwa jaani akiwa ndani ya gunia huku akikosa sehemu kadhaa za mwili wake.
Kuna wakati ambapo duru nyingi husema kuwa viuongo vya mwanadamu huuzwa ikiwemo macho ,vidole , figo nakadhalika , lakini je kutafuta maisha ni haki kumua binadamu mwenzako Kwa kutaka kutajirika.
Licha ya kwamba mashirika mengi hukemea hili suala la mauwaji ya wanawake na pia mwaka jana wanawake waliandamana kote nchini ili kushinikiza jamii kuacha kuwauwa kiholela ila bado kila siku visa hivi bado vinaendelea kuonekana.
Ni kwanini mara nyingi tunanyoshea kidole cha lawama kwa serikali wakati ambapo mauwaji yametokea?.je Raisi anahusika vipi na watoto kutupwa majaani? Raisi anahusika wapi wakati wanandoa wawili wanapoamua kukatiziana maisha?
Ili kuepuka lawama kama hizi Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yashirikiane kuelimisha jamii kuhusu thamani ya maisha na haki za binadamu.vilevile Sheria kali ziwekwe na kutekelezwa ipasavyo kwa wale wanaohusika na mauaji ya kiholela au utupaji wa watoto.
Wanawake wanaopata mimba zisizotarajiwa wapewe msaada wa kisaikolojia na kiuchumi ili kuwaepusha na maamuzi magumu kama kutupa watoto wao
Sote tujue kwamba matatizo kama haya yanapaswa kushughulikiwa kwa haraka na kwa nguvu zote.
Ni jukumu letu sote kusimama na kukemea uvundo huu wa ukatili ili kujenga jamii yenye huruma, haki, na usawa.
//Photo courtesy//
Muandishi: Hafsa Juma