Wanaharakati wapinga mchakato wakuajiri wafanyikazi Katika Bandari ya Mombasa (KPA)
By Dayo Radio
Published on 06/03/2026 15:30
News

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wamewasilisha malalamishi kwa mamlaka ya bandari mjini Mombasa (KPA) wakipinga mchakato unaoendelea wa kuajiri wafanyakazi katika taasisi hiyo.

Wanaharakati hao wakiongozwa na Ramadhan Beja, kutoka shirika la Midzi, amesema kuwa mchakato wa uajiri unaendelea kwa njia isiyo wazi na huenda ukakiuka kanuni za uwazi na usawa katika utoaji wa nafasi za kazi  na kudai kuwa kuna  haja ya mamlaka hiyo kusitisha zoezi hilo kwa muda ili kuhakikisha kuwa linafanyika kwa njia ya haki na inayofuata taratibu zote zinazotakiwa.

Kwa upande wake mwanaharakati Bradley Ouna  amemtaka mkurugenzi mkuu WA bandari  kusitisha mchakato huo Ili kuhakikisha na kutathmini vigezo vilivyotumika kuajiri watu kazi

Haya yanajiri baada ya umma kulalamika jinsi almashauri ya bandari mjini Mombasa huajiri wafanyikazi wake, wakidai  kazi hizo hutolewa Kwa njia ya ufisadi Hali ambayo huwa changamoto Kwa mwananchi wa  chini.

 

Comments
Comment sent successfully!