Baada ya kukamilika Kwa uchaguzi mkuu tarehe 9 mwezi Machi mwaka 2013, taifa la kenya llihamia rasmi kwenye mfumo wa utawala WA ugatuzi ambao ulianzishwa na Katiba mpya ya mwaka 2010.
Katiba mpya ilianzisha ngazi mbili za serikali ambazo ni Ile ya kitaifa na serikali 47 za kaunti.
Serikali hizi zina majukumu Maalum kisheria yaliyoanishwa katika sura ya Nne ya Katiba mpya.
Kenya ina wastani WA kilo mita mraba 246,757 za BARABARA.
Idadi hii inajumuisha barabara kuu chini ya serikali ya kitaifa, ambazo husimamiwa , hukarabatiwa, na kuendelezwa na mashirika ya kitaifa ya barabara.
Vile zipo barabara za kaunti ambazo hutengenezwa na kudumishwa na serikali za kaunti husika.
Kwa sasa, Serikali ya Kitaifa ina jukumu la kudumisha kilomita 44,021 za barabara, ambazo zimeainishwa kama barabara kuu za kitaifa huku serikali za kaunti zikiwajibika kwa kilomita 118,034 za barabara zilizoainishwa kama barabara za kaunti.
Tangu ujio wa mfumo wa ugatuzi 2013 Serikali za kaunti ya Mombasa imekuwa ikifanikisha ujenzi wa barabarani kuwa kichocheo kikuu cha maendeleo ya kiuchumi.
Idara ya uchukuzi na miundombinu katika kaunti ya Mombasa ina jukumu la kujenga na kuzisimamia barabara, kuhakikisha mfumo Bora wa upitishaji maji taka pamoja na kuweka taa za "mulika mwizi" katika Barabarani na vitongoji.
Serikali kaunti ya Mombasa imekuwa likitanguliza maendeleo ya barabara kwa kutenga bajeti kubwa ili kufaNIkisha Oparesheni katika sekta HII
Kufikia sasa Serikali ya Kaunti ya Mombasa imejenga barabara zaidi ya kilomita 100 katika kaunti katika maeneo bunge yote kama njia mojawapo ya , kuimarisha usalama na kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
Miongomi mwa miradi ya miundo msingi ambayo imefanikishwa na serikali ya kaunti ni pamoja Ukarabati wa Daraja la Aldina-Kwa Ng’ombe Drift ENEO bunge Jomvu ambao umeimarisha usalama na maendeleo ya kiuchumi na utangamano wa kijamii.
Aidhaa taa zilizowekwa katika makutano ya Saba Saba, Buxton, Kengeleni, Digo, Makadara na King’orani zimepunguza msongamano wa magari na kuimarisha pakubwa usalama.
Mbali na hayo, Kwa muda Swala la upitishaji mfumo WA maji taka yaani drainage system limekuwa jinamizi katika kaunti ya Mombasa.
Hatahivyo kupitia ugatuzi serikali ya kaunti ya Mombasa imejenga mifumo mipya WA usambazaji MAJI taka katika maeneo ya Majengo, Barabara ya Old Malindi,, Sisi kwa Sisi, Flamingo, Wayani, Mwijabu Primary, Likoni. magorofa, miongoni mwa maeneo mengine.
Licha ya kwamba mfumo WA ugatuzi unakabiliwa na changamoto nyingi NCHINI,Kaunti ya Mombasa ni Miongoni kaunti ambazo zimejitahidi Kwa kiasi kikubwA kuhakikisha Kuwa mfumo huu unafanikiwa HUSUSAN katika Idara ya uchukuzi na miundo msingi .
Idara hiyo inaendeleza miradi Mbali Mbali katika maeneo bunge yote sita,lengo likiwa kurahisha uchukuzi na kukuza uchumi WA kaunti ya Mombasa.
LICHA YA KUWA mfumo WA ugatuzi UMEAFIKIA mengi katika MASUALA ya maendEO,
gavana WA KAUNTI YA MOBASA ABDULSWAMDA SHARIFF NASSIR SI MARA MOJA ameonya kwamba mfumo huo huenda ukaSAMBARATIKA Endapo serikali itaendelea kuchelewesha usambazaji wa Fedha kutoka serikali KUU.
VILE AMEKUWA GAVANA HUYO AKIISHINIKIZA SERIKALI NYONGEZA YA MGAO WA FEDHA KWA SERIKALI ZA KAUNTI ILI KUHAKIKISHA KUWA KAUNTI ZINATEKELEZA MIRADI PASI NA CHANGAMOTO ZOZOTE
Ni Dhahiri Shahiri kwamba Serikali ya kaunti ya Mombasa imepiga hatua kubwa katikA UJENZI WA Barabara na kukarabati miundo msingi mipya.
Ni jitihada ambazo zimepongezwa na wakaazi wakiutaja ugatuzi Kuchangia mafanikio hayo
.Hatahivyo licha ya hatua hizo, kizingiti kikuu katika kufanisha miradi ZAIDI ya miundo msingi kwenye KAUNTI hii Swala la UKOSEFU WA Fedha huku WITO Kwa SERIKALI ya kitaifa Kufanya HIMA na kusambaza Fedha za kaunti Kwa wakati Ili kuepusha kukwamisha miradi hii ya maendeleo.
story by HAFSA JUMA