UTABIRI WA HALI YA HEWA MOMBASA
By Dayo Radio
Published on 26/02/2026 13:28
News

Na Elijah Muthini 

Hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya mchanganyiko katika kipindi chote cha wiki (24 Februari-2 Machi) huku kunatarajiwa kuwa jua kali na mvua za rasharasha za asubuhi. Baadhi ya maeneo yanatarajiwa kushuhudia mvua za asubuhi, hivyo ni vyema kubeba mwavuli unapokwenda kazini au shuleni.

Joto la mchana litabaki kuwa la juu huku likitarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 31–33°C, huku joto la usiku likiwa takribani nyuzi joto 25°C.

Upepo wa wastani wenye kasi ya mita 5 hadi 7 kwa kila sekunde unatarajiwa kuvuma ukisaidia kupunguza makali ya joto na kuleta hali ya ubaridi.

Kwa wanaopanga shughuli katika ukanda wa Pwani kuna habari njema, hali ya bahari inatarajiwa kuwa tulivu, ikiwa na urefu wa mawimbi kati ya mita 0.4 hadi 1.2 hali inayofaa kwa uvuvi, usafiri wa baharini pamoja na shughuli za burudani. Wananchi wanashauriwa kuwa makini barabarani wakati wa mvua za asubuhi.

Comments
Comment sent successfully!