Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga amefariki dunia nchini India alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Devamatha.
Kulingana na Daktari mkuu wa moyo wa hospitali hiyo Dkt. Alphonse, amesema Raila alikuwa akisumbuliwa na kisukari, shinikizo la damu, pamoja na ugonjwa sugu wa figo.
Dkt. Alphonse ameeleza kuwa madaktari walijaribu kumwokoa kwa kutumia mbinu ya urejeshi wa mapigo ya moyo na upumuaji almaharufu, "cardiopulmonary resuscitation" (CPR) na mbinu nyingine za dharura, lakini juhudi zao hazikufanikiwa.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo Alhamisi, tarehe 16 Oktoba 2025, kwa maandalizi ya mazishi ya kitaifa.
Kifo cha Raila kimeibua vumbi la huzuni na rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani, wakimtaja kama mwana-demokrasia na kiongozi mashuhuri wa Afrika.