KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU KILIMO CHA MAKUBALIANO (ICCF 2025) KUFANYIKA SIKU YA KESHO -NAIROBI.
By Dayo Radio
Published on 17/11/2025 19:14
News

Kongamano la Kimataifa kuhusu Kilimo cha makubaliano (International Conference on Contract Farming – ICCF 2025) linatarajiwa kufanyika siku ya kesho tarehe 18–19 Novemba 2025 Westlands jijini Nairobi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari kongamano hilo linatarajiwa kuwakutanisha washikadau muhimu wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima, wajasiriamali wa kilimo (agripreneurs), watunga sera, wawekezaji, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), wavumbuzi wa teknolojia za kilimo (agri-tech innovators), pamoja na washirika wa maendeleo ili kujadili na kuweka mikakati thabiti ya kuimarisha mfumo wa contract farming nchini na kote ulimwenguni.

Kwa mujibu wa waandaaji wa kongamano hilo ni kwamba linatarajiwa kutoa dira mpya itakayowezesha wakulima na wawekezaji kunufaika kwa usawa, kuboresha misingi ya mikataba ya kilimo, kuongeza upatikanaji wa masoko, kuimarisha uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuchochea matumizi ya teknolojia katika uzalishaji wa kisasa.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!