Sura ya nne ya katiba ya Kenya Kifungu cha 43 ibara ya kwanza (a) inampa kila mwananchi haki ya kupata viwango vya juu vya afya.
Aidha kifungu cha 27 cha Katiba pia kimebainisha Kuwa kila mtu, ikijumuisha wanaougua ugonjwa WA kifafa Wana haki sawa ya kulindwa na kunufaika na matibabu ya viwango vya Hali ya juu
Lakin je vifungu hivi vya sheriah vinatekelezwa kikamilifu humu nchini ?
Maradhi ya kifafa ni Ugonjwa ambao unasababishwa na kufaidhaika kwa seli za ubongo na kusababisha mshtuko. Vile vile Kifafa kinaweza kutokea kama matokeo ya ugonjwa, maumbile au jeraha la ubongo, kama vile kiwewe au kiharusi yaani stroke.
Utafiti uliofanywa na shirika la afya duniani WHO unaonyesha kwamba watu millioni 50 ulimwenguni wanaugua maradhi ya kifafa.
Mara nyingi jamii huona maradhi haya kama laana fulani ,au mapepo pasi na kujua ni moja wapo ya ulemavu au maradhi ambayo yanafaa kutibiwa hospitalini na Wala hauhusiki na maswala ya kishirikina
Jamii ya watu wenye maradhi haya wanapata changamoto nyingi sana kiasi cha kukosa huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini.
Katika kaunti ya mombasa , ukosefu wa huduma za kifafa ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazoshuhudiwa . Utafiti unaonyesha kwamba kuna dakatari mmoja pekee katika kaunti nzima ya mombasa ambaye anashugulikia masuala ya kifafa, hali inayowaweka kwenye hatari kubwa jamii ya watu wanaougua maradhi haya.
Simon kakawa ni mmoja wa wale wanaougua maradhi haya,vile vile ni kiongozi katika kikundi cha saidia people with epilepsy amesema kwamba kupata huduma za kifafa kaunti ya mombasa ni changamoto moto kwao sana hali inayowapelekea kufuata huduma hizo ikiwemo dawa katika kaunti Jirani ya kilifi.
"Katika kaunti ya mombasa hakuna dawa wala madakitar wakutosha inatubudi kuenda kutafuta huduma hizi kilifi ,licha yakwamba tunapata huduma hizo bure kilifi lakin wengi wetu hawawezi kufika uko sababu ya kukosa pesa"
Vilevile amebainisha kwamba gharama ya kufanyiwa vipimo vya kifafa ni ghali mno, maana mtu anahitajika kuwa na takriban sh.9000 ndiposa apate vipimo hivyo hali inayowapelea wengi wao kukosa kupata vitambulisho vya kuonyesha kuwa wao ni walemavu wa kifafa
"Kuna baadhi ya hospital ambazo wanapeana vipimo vya kifafa .lakin ni bei ghali sana takriban shilling 9000 .hali ambayo inafanya baadhi yetu pia kukosa vitambulisho vya kuwa wao na walemavu na kukosa kithibitisho hicho inawafanya wao kukosa kupata misaada pia katika jamii.sababu kupata vitambulisho hivyo mpaka uwe unafanyiwa vipimo na dakatari."
Ziro kahati ambae ni muhudumu wa afya katika hospital ya ziwa la ngombe kaunti ya Mombasa amesema kuwa maradh yakifafa ni maradhi ambayo wengi huzaliwa nayo na baadhi huyapata baadae, na hayahusiki Kwa vyovyote vile ma maswala ya ushirikina .Anasema ni maradh ambayo yanafaa kutibiwa hospitalini.
"Maradhi ya kifafa ni maradh kama mengine tu, jamii iache dhana potofu kuwa ni ushirikina au mapepo.wapeleke wagonjwa hospitalini ili wapate huduma kwa muda unaofa ili kuepuka madhara zaidi"
Kadhalika kahati amekiri kuwa maradhi ya kifafa yanachangamoto nyingi sana hasa katika kupata huduma za afya
Amesema hospital nyingi katika kaunti ya mombasa hazitoi huduma hizo huku akiiomba serikali kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ili waweze kukabilina na maradhi hayo
"Ningeoiomba serikali ilete mafunzo nyanjani kwa wahudumu wa afya ili tuweze kufahamu njia zakuwashughulikia wagonjwa wenye maradhi haya.vile vile walete vifaa muhimu vya kuifanyia vipimo vya wagonjwa hawa"
Dream achieves youths organization ni shirika ambalo linajihusisha pakubwa na masuala ya ulemavu.Kulingana na enos opiyo ambae ni mmoja wa waratibu katika shirika hili amesema kwamba kama shirika wanajitajidi vilivyo kuwatafutia haki watu wenye kifafa.
licha ya kwamba shirika hili halina uwezo kamili wa kuwaletea madakatri kuwatibu wagonjwa wa kifafa, Enos Amesema kwamba Bado wanaendeleza sera za haki ya jamii wenye kifaf Ili kuweka hamasisho vile vile kuisaidia jamii ya wanaougua ugonjwa huu kupata wafadhili wanaoshugulikia masuala haya.
"Kama shirika tunawasidia wagonjwa wa kifafa katika kupata wafadhili wanaoshugulikia masuala ya walemavu ili wapate usaidizi.vile vile tunawasaidia katika kupaza sauti za kutafuta haki zao zakupata huduma za afya mjini mombasa ."
Wasemao husema ulemavu si uchawi bali ni maajiliwa yake mwenyezi mungu.hakuna apendaye kuzaliwa na kasoro lakin ni hali ambayo hatuewezi kuiepuka
Ni jukumu la vitengo vya afya vikishirikiana na serikali kuu pamoja nazile za kaunti kuhakikisha usawa wa huduma za afya unatekelezwa kama ilivyoainishwa kwenye katiba Ili kuhakikisha Kuwa wanaougua ugonjwa wa kifafa wanapata matibabu wanayohitaji.
Msimulizi amekuwa wako,
HAFSA JUMA