Miongoni mwa miezi kumi na mbili ya mwaka , kunazo siku maalumu ambazo huadhimishwa humu nchini kwa sababu Mahususi.
siku hizo kuidhimishwa kutokana na matukio ya kipekee yanayofanyika katika siku hizo.Miongoni mwa hizi siku ya mazingira day.
Siku hii huadhinishwa Kwa Kupanda miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na majanga mengine kama vile ukame ,baa la njaa Miongoni mwa mengine.
Hapo awali siku hii ilikuwa akifahamika kama moi day , ili kumuenzi Rais wa zamani wa Kenya hayati Daniel Moi.
Kufuatia kurasmishwa kwa Katiba mpya ya Kenya mnamo Agosti 2010, Siku hii ilifanyiwa marekebisho na kuitwa jina la mazingira day .
Kutokana na majanga ya mabadiliko ya tabia nchi, siku hii maalumu ilibadilishwa kutoka moi day hadi mazingira day ili kuhamasisja upanzi WA miti , na kufanya mambo mengine kadha wakadha yatayosaidia katika kupambana na hali hii.
Ukataji wa miti nchini , ni moja kati ya donda sugu ,linashuhudiwa kila uchao, viongozi mbali mbali pamoja na taasisi husika wamekuwa wakitoa nasaha na mafunzo mengi kuhusu umuhimu wa kupanda miti lakin wengi wao hufanya kinyume cha kila wanachokatazwa.
Miezi kadhaa iliyopita , familia nyingi zilipoteza wapendwa wao kutokana na mvua kubwa iliyokua ikishudiwa, familia pia zilikosa makazi na hata Kwa WANAFUNZI masomo hayakueza kuendelea.
Si haya pekee bali hata msimu wa baridi kali yaani kimbuga bado haikua rahisi kukabiliana na kadhia hizi.
Wengi wetu tulinyooshea kidole cha lawalama kwa serikali Kwa tuhuma za utendakazi duni.Aidha Duru ziliarifu Kuwa pesa za kukabiliana na kadhia hizi zilifisadiwa.
Kimtazamo wa mambo ya yalivyo ,JE SERIKALI INAWEZA KUKABILIANA NA TABIA NCHI AU INAHUSIKA VIPI KWA KUNYESHA KWA MVUA NYINGI ,BARID KUUBWA NA HATA KIANGAZI.
wahenga walinena kwamba kidole kimoja hakivunji chawa ,serikali ni kidole kimoja ,vyengine tiisa ni sisi tunayoishi navyo, tuache kufanya mambo yasiyostahiki bali tufanye yale yenye manufaa na kheri kwetu na vizazi vijavyo.
Serikali inapania kufikisha miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2030, ili kufanisha haya , tuungane pamoja tujenge nchi yetu.
tushiriki sote katika upanzi wa miti pamoja na mipango mengi ya serikali itakayoweza kudhibiti tabia nchi siku za usoni.
Ukosefu wa mvua , kiangazi ,mafuriko , njaa yote dawa ni kupanda miti,
Tushiriki sote katika kuadhimisha siku ya mazingira day nchini ambayo ni tarehe kumi mwezi wa kumi ,tujitahidi kupanda miti ijapo mmoja pekee Kwa sababu haba na haba hujaza kibaba , Ili tuweze kuwapatia maisha mazuri vizazi vijavyo ,ni matendo ya wakati tulionao ndio yatakayotegemea
Ikumbukwe kufikia kiwango cha miti billioni 15 sio kazi rahisi lakini Endapo tushirikiana tutafanikisha utandu WA misitu nchini kupitia ushirikiano HUO.
wasemao husema safari ya kesho hupangwa leo na KIDOLE kimoja hakivunji chawa.
Kazi kwetu!
BY:HAFSA JUMA