WASANII WA PWANI WAIOMBA SERIKALI KUU NA ZA KAUNTI KUFADHILI SANAA.
By Dayo Radio
Published on 15/09/2025 15:34
Entertainment

Wasanii Kutoka Kaunti ya Mombasa sasa wanaitaka serikali Kuu na pia serikali za Kaunti Ukanda wa Pwani Kufadhili sanaa Kama njia mojawapo ya Kupiga jeki sekta hiyo muhimu ya Michezo na sanaa.

Wakizungumza na waandishi wa Habari Mjini Mombasa wakati wa hafla iliyoandaliwa na Baraza Media Lab, wasanii hao, wakiongozwa na mwasisi wa shirika la uchoraji la BigFootArts Hudson Sabala wamelalamikia kutelekezwa na serikali.

Hata hivyo Hudson Sabala ameshukuru shirika la Baraza Media Lab Kwa kuwapa jukwaa mwafaka wasanii chipukuzi ili kuelimisha na kuhamasisha Jamii Kuhusu maudhui mbali mbali kupitia sanaa.

Kwa upande wake mratibu wa Programu Baraza Media Lab Wanjiru Nguhi amesema kwamba wataendelea Kuwapa wasanii nafasi ya Kujieleza Kwa umma kupitia sanaa huku akiwarahi vijana kukumbatia sanaa Kukuza talanta zao, kujiajiri na pia kujikimu kimaisha 

"Tumetelekezwa na serikali, lakini tunashukuru Baraza Media Lab kwa kutupa jukwaa mwafaka la kuelimisha na kuhamasisha jamii kupitia sanaa."

Kauli yake Wanjiru imeungwa Mkono na Matie Mtange ambaye amesema Baraza Media Lab itazidi kupanua wigo sehemu tofauti nchini ili kuwafikia wasanii na Kuwapa jukwaa mwafaka la Kujieleza Kupitia sanaa. 

"Tutaendelea kuwapa wasanii nafasi ya kujieleza kwa umma kupitia sanaa huku tukiwarai vijana kukumbatia sanaa kukuza talanta zao, kujiajiri na pia kujikimu kimaisha."

Ufunguzi Rasmi wa ukumbi wa sanaa wa Baraza Media Lab Mjini Mombasa umeratibiwa kufanyika Baadaye mwezi huu wa Septemba.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!