RAPA MKALI WA PWANI MASTER KIMBO APATA BARAKA YA MTOTO WA KIKE
By Dayo Radio
Published on 12/06/2025 07:18
Entertainment

Rapa maarufu kutoka Pwani ya Kenya, Master Kimbo, ameanza ukurasa mpya katika maisha yake ya kibinafsi baada ya kujaliwa kupata mtoto wa kike. Kupitia ukarasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, msanii huyo aliandika kwa furaha:

"Welcome to the world my daughter Alyah."

 

Habari hizi zimepokelewa kwa bashasha na mashabiki wake pamoja na wadau wa muziki kote nchini, wakimtumia pongezi na baraka tele kwa zawadi hiyo adhimu.

 

Master Kimbo ni jina linaloheshimika kwenye tasnia ya muziki wa hip hop na rap nchini Kenya, hasa katika Ukanda wa Pwani. Ametambulika kwa ubunifu wake na midundo ya kipekee, huku kibao chake maarufu "English Gold" kikiendelea kufanya vizuri katika majukwaa ya muziki hata baada ya miaka kadhaa tangu kutolewa kwake.

 

Ingawa mashabiki wamegundua kuwa hatowi nyimbo kwa kasi kama zamani, Kimbo ameendelea kuwa mstari wa mbele kwenye matamasha makubwa, hasa nyakati za msimu wa sherehe, akiburudisha maelfu ya wapenzi wa muziki.

 

Kupata mtoto ni hatua kubwa na yenye maana katika maisha ya mtu yeyote, na kwa Master Kimbo, ni wazi kuwa tukio hili limeleta furaha na msukumo mpya. Katika jamii ya wasanii na mashabiki wake, tukio hili limetafsiriwa kama mwanzo wa sura mpya ya maisha — si tu kama msanii, bali pia kama mzazi.

 

Ombi kwa Jamii

 

Katika hali ya utu na upendo, tunamuombea mtoto wa Master Kimbo, Alyah, awe na maisha marefu yenye afya, hekima na mafanikio. Tunatumai kuwa atakuwa baraka si tu kwa familia yao, bali pia kwa jamii nzima.

 

Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kuona ni namna gani tukio hili litamchochea Kimbo kuja na kazi mpya zenye maudhui ya kina zaidi, yakichora taswira ya maisha yake mapya kama baba.

Comments
Comment sent successfully!