UTABIRI WA HALI YA HEWA.
By Dayo Radio
Published on 21/07/2026 15:50
News

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini imesema hali ya hewa ya mchanganyiko pamoja na upepo inaendelea kutarajiwa katika kipindi cha wiki hii kuanzia Julai 21 hadi 27, 2026.

Kwa mujibu wa utabiri huo, baadhi ya maeneo yanapata mvua nyepesi za asubuhi katikati na mwishoni mwa wiki. Joto la mchana linakadiriwa kuwa kati ya nyuzi joto 29 hadi 31 Selsiasi, huku joto la usiku likiwa wastani wa nyuzi joto 23 Selsiasi.

    

Aidha, upepo wa wastani hadi mkali kutoka kusini unaendelea kuvuma, huku hali ya bahari3 ikitarajiwa kuwa ya wastani hadi yenye mawimbi makubwa.

Wananchi, hususan wavuvi, waendesha boti na watumiaji wengine wa bahari, wameshauriwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa kabla ya kuingia baharini na kuepuka safari zisizo za lazima wakati wa upepo mkali au mawimbi makubwa.

Comments
Comment sent successfully!