NAIBU GAVANA FLORA MBETSA CHIBULE AONGOZA UZINDUZI WA MACHAPISHO YA NGEC NA UTOAJI WA TUZO ZA USAWA AWARDS 2026 KILIFI.
By Dayo Radio
Published on 28/07/2026 13:00
News

Naib gavana wa kaunti ya Kilifi, Flora Mbetsa Chibule, ameongoza hafla ya uzinduzi wa machapisho ya National Gender and Equality Commission (NGEC) pamoja na sherehe ya utoaji wa USAWA Awards 2026 iliyofanyika katika ukumbi wa CDA Kilifi. Hafla hiyo imewakutanisha viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo, mashirika ya kiraia na wananchi katika kuendeleza ajenda ya usawa, haki na ujumuishaji wa kijamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Gavana amesisitiza kuwa usawa wa kijinsia ni msingi wa maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.

   

"Hatutaweza kufikia maendeleo ya kweli ikiwa tutawaacha nyuma wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi. Ni jukumu letu kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa sawa za kushiriki na kunufaika na maendeleo," amesema Flora Mbetsa Chibule.

Aidha, amewapongeza washindi wa USAWA Awards 2026 kwa mchango wao katika kukuza usawa, kutetea haki za binadamu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa ujumuishaji.

"Tuzo hizi zinatambua juhudi za wale wanaosimamia haki na usawa katika jamii. Tunapaswa kuendelea kushirikiana ili kujenga jamii yenye usawa, heshima na fursa kwa wote," ameongeza.

Hafla hiyo imehitimishwa kwa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, taasisi za umma, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha sera na mipango inayolenga usawa na haki inatekelezwa kikamilifu kwa manufaa ya wananchi wote bila ubaguzi.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!