Mwanamuziki maarufu wa Taarab kutoka Tanzania, Khadija Kopa, amethibitisha kuwa binti yake ambaye pia ni nyota wa Bongo Fleva, Zuchu, ameolewa rasmi na mkali wa muziki Diamond Platnumz.
Khadija Kopa amefunguka kuhusu ndoa hiyo ambayo ilikuwa inazungumziwa kwa muda, na ametuma baraka zake kwa wanandoa hao wapya.
Katika picha iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Khadija Kopa alionekana akiwa pamoja na Mama Dangote, mama mzazi wa Diamond, ishara nyingine kuwa familia zimeungana rasmi kupitia ndoa hiyo.
Na Rajab Waziri