Msanii Billnas amezua gumzo mtandaoni baada ya kutoa maoni kuhusu rangi ya pink, akisema kuwa "Kuna haja ya bendera yetu kuongezewa rangi ya pink", kauli iliyokuja baada ya yeye kushona vazi la rangi hiyo kwa ajili ya harusi ya msanii mwenzake Jux nchini Nigeria.
Kauli hiyo imeibua maoni tofauti mitandaoni—wengine wakiona kama ni utani wa kawaida wa kisanii na mitindo, huku wengine wakichukulia kwa uzito zaidi wakisema bendera ni alama ya taifa isiyopaswa kubadilishwa kirahisi.

Kwa upande mwingine, Billnas anaonekana kutumia jukwaa hilo kuendeleza mazungumzo kuhusu mitindo na uhuru wa kujieleza, hasa kwa wanaume kuvaa rangi ambazo zamani zilionekana kama za kike.
Unadhani alikuwa serious au ilikuwa tu njia ya kuchekesha na kuonyesha support kwa Jux?