Willy Paul Amchokoza Eric Omondi Kuhusu Maisha ya Mahusiano
By Dayo Radio
Published on 10/04/2025 06:09
Entertainment

Msanii wa muziki Kenya Willy Paul, amezua mjadala mtandaoni baada ya kumchokoza mchekeshaji Eric Omondi kupitia kauli ya utani mzito. Kupitia maoni kwenye video ya Eric, Willy Paul aliandika: “Unapiga content sana bro, jana uliachwa ama hauna habari?”

Kauli hiyo ilizua vicheko na mijadala miongoni mwa mashabiki, wengi wakichukulia kama mzaha wa kawaida wa mastaa wanaotambiana kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walihoji kama kuna ukweli wowote kuhusu hali ya mahusiano ya Eric Omondi, huku wengine wakimpongeza kwa kuendelea kutoa burudani bila kuchoka.

Willy Paul na Eric Omondi wamekuwa na historia ya kuchokozana kwa njia ya vichekesho na kejeli za kirafiki, jambo linalowafanya wawe gumzo mara kwa mara kwenye mitandao

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online