Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na wawili hao zinaeleza kuwa si tu wameamua kurudiana, bali pia wamepata baraka na radhi kutoka kwa wakubwa wanaowaheshimu, jambo lililokuwa kikwazo awali. Hii imeongeza matumaini ya kudumu kwa uhusiano wao mpya.

Wakati mashabiki wakifuatilia kwa karibu kila kinachojiri, wawili hao wanaonekana kuushika moyo wa jamii kwa upya, wakionesha kuwa mapenzi ya kweli huweza kushinda mitihani ya muda na majaribu ya maisha.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kadri tunavyopokea kutoka kwa vyanzo vyetu vya kuaminika.