Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ametajwa kulipwa dola 600,000 (zaidi ya TSh bilioni 1.5) kutumbuiza kwenye sherehe ya kifahari ya kuzaliwa ya bilionea wa Ghana, Richard Niamah.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ghpage, Diamond aliweka rekodi kwa kuwa msanii aliyeongoza kwa malipo, akifuatiwa na Davido kutoka Nigeria aliyelipwa dola 500,000 (zaidi ya TSh bilioni 1.2). Wasanii nyota wa Ghana, Sarkodie na Stonebwoy, walilipwa dola 200,000 (takribani TSh milioni 500) kila mmoja.

Tukio hilo limeonesha wazi jinsi muziki wa Afrika Mashariki, hususan Bongo Fleva, unavyozidi kuvuka mipaka na kuthibitisha hadhi ya Diamond kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Hii si mara ya kwanza kwa Diamond Platnumz kupata malipo makubwa katika maonesho ya kimataifa, jambo linaloimarisha nafasi yake kama msanii wa daraja la juu katika tasnia ya burudani.

Mashabiki na wadau wa muziki wameendelea kumpongeza Diamond kwa mafanikio haya, wakitaja juhudi zake za kujituma na uwekezaji mkubwa katika muziki wake kama nguzo muhimu ya mafanikio hayo.