Diamond Platnumz Asajili Msanii Mpya Baada ya Kuondoka kwa Mbosso
By Dayo Radio
Published on 23/03/2025 07:46
Entertainment

 

Mwimbaji mkongwe wa Tanzania, Naseeb Abdul Juma Issack, maarufu kama Diamond Platnumz, ametangaza kumsajili msanii mpya chini ya lebo yake ya Wasafi Records. Tangazo hili limekuja siku chache tu baada ya Mbosso, aliyekuwa mmoja wa wasanii wa muda mrefu wa lebo hiyo, kutangaza kuondoka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond alishiriki picha ya mkataba uliotiwa saini Machi 18, 2025, kati ya Wasafi na msanii huyo mpya. Akiambatanisha na maneno "Icon mpya inakuja," alidokeza ujio wa kipaji kingine kipya kwenye tasnia ya muziki.

Hadi sasa, jina la msanii huyo bado halijawekwa wazi, lakini mashabiki wa Wasafi Records wanatarajia kutangazwa rasmi hivi karibuni.

Tunasubiri kuona ni nani ataongeza nguvu katika familia ya Wasafi na jinsi atakavyoleta mapinduzi kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online