SANAIPEI TANDE: "SIWEZI KUBUSU KWENYE MOVIE WALA KUVAA NUSU UCHI!"
By Dayo Radio
Published on 17/03/2025 20:24
Entertainment

Msanii maarufu wa muziki na filamu, Sanaipei Tande, amefunguka wazi kuhusu mipaka yake anaposhiriki katika filamu. Akiweka msimamo wake, amesema hawezi kubusu kwenye lips, kuvaa mavazi yanayoonyesha mwili wake kupita kiasi, kuigiza kama mpenzi wa jinsia moja (LGBTQ), wala kushiriki katika tukio la ngono kwenye filamu yoyote.

Sanaipei, anayeheshimika kwa kipaji chake na msimamo thabiti, amesema kuwa anaheshimu sana maadili yake na hawezi kwenda kinyume na misingi anayoamini. Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, huku mashabiki wakitoa maoni tofauti kuhusu maamuzi yake.

Wewe unahisi vipi kuhusu wasanii kuweka mipaka kwenye kazi zao?

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online