Published on 12/03/2025 by Dayo Radio
Tasnia ya muziki na burudani imepata pigo kubwa baada ya kifo cha msanii mchanga Liz Kamene, anayefahamika kama Icon KE, mwenye umri wa miaka 22. Icon KE ameaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Kariobangi, Nairobi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Icon KE alipata ajali wakati akijaribu kuwafukuza wezi waliokuwa wamemuibia simu yake. Juhudi zake za kurejesha mali yake ziligonga mwamba baada ya kugongwa na gari, na juhudi za kumuokoa hazikufua dafu.

Icon KE alikuwa msanii mwenye kipaji kikubwa aliyekuwa akijipatia umaarufu kwa kazi zake za ubunifu katika muziki na sanaa. Kifo chake kimewaacha wengi na majonzi, hasa mashabiki na marafiki waliokuwa wakifuatilia safari yake ya mafanikio.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi na shughuli za kumbukumbu zitatolewa na familia yake. Dunia ya burudani imempoteza nyota anayechipukia, lakini urithi wake utaendelea kuishi kupitia kazi