Vera Sidika Amtafuta Mwanamume Aliyemwahidi Kula Bata Naye Akishinda Jackpot
Sosholaiti mashuhuri Vera Sidika ameanza msako wa kumtafuta mwanamume aliyewahi kumwahidi kwamba watakula bata pamoja iwapo atashinda jackpot ya shilingi milioni moja.
Kupitia ujumbe wake, Vera alieleza kuwa mwanamume huyo alimfikiria kabla ya familia yake, jambo ambalo limemgusa pakubwa. "Nitampeleka matembezi kwa chakula cha mchana. Alinifikiria mimi kabla ya familia yake," alisema Vera kwa msisitizo.
Hata hivyo, hajafichua jina wala maelezo zaidi kumhusu mtu huyo, lakini mashabiki wake wamesisimka na wengine wakijitokeza wakidai kuwa wao ndio wahusika.
Mashabiki wanangoja kuona iwapo Vera atampata mwanamume huyo na kutimiza ahadi yake.