Mwakilishi wadi wa shanzu eneo bunge la kisauni kaunti ya Mombasa Allen Katana,amesema kwamba amekuwa akipokea jumbe za vitisho kutokana na juhudi zake za kuzuia mabwenyenye kunyakua ardhi za wa pwani.
Akizungumza hapo Jana katika mkutano na wakazi wa eneo bunge la kisauni katika uwanja wa shule ya msingi ya utange,katana amesema kwamba seneta wa Mombasa Mohamed Faki,amekuwa akimtumia jumbe za vitisho Kwa juhudi zake za kutetea wakazi wanaopoteza mashamba Yao kupitia Kwa mabwenyenye huku akimhusisha senata huyo kuwa Mmoja wa mabwenyenye anayetumia wadhfa wake kama wakili kunyanyasa wakazi wa kisauni.
"Nimekuwa nikihangaishwa kupitia jumbe za vitisho kutokana na juhudi zangu za kuzuia mabwenyenye kunyakua ardhi za wenyeji wa Pwani. Seneta wa Mombasa, Mohamed Faki, amenitumia jumbe za vitisho kwa sababu ya kupigania haki za wakazi wanaopoteza mashamba yao. Ninamhusisha seneta huyu kuwa miongoni mwa mabwenyenye wanaotumia nyadhifa zao kama mawakili kuendeleza unyanyasaji dhidi ya wakazi wa Kisauni."
Haya yanajiri wakati wakazi wa pwani wamekuwa wakiishi maisha uskota tangu jadi hali ambayo imewafanya kukosa hati miliki zitakazowasaidia katika mikakati ya kufanya maendeleo na kujikuza kiuchumi.
NA HARRISON KAZUNGU