Serikali ya kaunti ya Mombasa imeapa kuwachukulia hatua Kali za kisheria watu wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya uwizi wa maji.Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za maji ,gavana wa Mombasa Abdulswamad sharrif nassir amesema kwamba Kuna visa takribani 21 vya uunganishaji wa maji kinyume cha Sheria katika kaunti ya Mombasa.
Gavana nassir nassir amefichua kwamba baadhi ya watu hao ni wafanyikazi wa serikali ya kaunti na wengine wa serikali kuu. Gavana huyo sasa ametishia kuwachukuliwa hatua Kali za kisheria watu hao Kwa kuhujumu usambasaji wa maji Kwa wakaazi wa Mombasa.
Wakati uo huo gavana nassi amewarai wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana na wadau husika katika kufichua watu ambao wanajihusisha na wizi wa maji.
“Tumeweza kubaini visa takribani 21 vya uunganishaji wa maji kinyume cha sheria hapa Mombasa, na baadhi ya wahusika ni wafanyikazi wa kaunti na wengine wa serikali kuu. Tunataka kuwaambia wazi kwamba tutawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuhujumu usambazaji wa maji kwa wakaazi wa Mombasa. Nawaomba wakazi washirikiane na wadau kufichua wote wanaojihusisha na wizi huu wa maji.”
Kauli ya gavana inajri huku kaunti ya Mombasa ikishuhudia upungufu na uhaba wa maji Kwa takribani miezi 2.