Polisi eneo la Lurambi kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mwanamume wa umri takriban 55, anadaiwa kuaga dunia katika hali ya kutatanisha ndani ya chumba cha kukodi katika eneo moja la burudani.
Taarifa za awali zinadai kuwa jamaa huyo aliaga dunia baada ya kutumia dawa za kusisimua misuli wakati wa tendo la ngono na msichana waumri wa miaka 24.
Mmiliki wa hoteli hiyo amesema kuwa maiti ya mzee huyo ilipatikana mwendo wa saa moja usiku wakati mfanyakazi alipoingia chumabni humo na kupata mzee huyo akiwa amelala sakafuni huku msichana huyo asijulikane aliko.
Kwa sasa, wakaazi wameitaka serikali kupiga marufuku dawa zinazodaiwa kutumiwa na wanaume haswaa wazee wakati wanaposhiriki tendo la ngono.