KCSE KUMALIZIKA WIKI HII
By Dayo Radio
Published on 16/11/2026 15:10
News

Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne wa KCSE umeingia  wiki ya tano na ya mwisho huku watahiniwa wakifanya mitihani ya mwisho ya masomo ya nadharia kabla ya kukamilika kwa mitihani hiyo siku ya ijumaa.

Jumla ya watahiniwa milioni moja elfu mbili na nane na hamsini na tano walijiandikisha na kufanya mtihani huo ulioanza tarehe kumi na tisa mwezi jana. 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na baraza la kitaifa la mitihani nchini KNEC watahiniwa watafanya leo mtihani wa Jografia, Fizikia na sayansi ya jumla,hapo kesho Jumanne watahiniwa hao watafanya mitihani ya masomo ya biashara na kilimo kabla ya kufanya mtihani wa pili wa jografia na fizikia siku ya Jumatano. 

Hata hivyo idadi ya watahiniwa wanaofanya mtihani huo imepungua kufuatia taarifa za baadhi ya watahiniwa kutohudhuria mitihani pamoja na vifo vilivyoripotiwa katika kipindi cha mitihani.

Comments
Comment sent successfully!