Serikali imewaonya watu wanaotumia picha au video na taarifa binafsi za watoto walio katika mazingira magumu mitandaoni kuomba michango au kutangaza shughuli za uhisani.
Kupitia idara ya huduma za watoto wizara ya jinsia utamaduni na huduma kwa watoto wamesema kuwa ,licha ya juhudi ya kuwasaidia watoto hao ni lazima wahisani waheshimu utu na faragha ya watoto.
Aidha idara hiyo imewataka wote waliojitokeza kama wahisani ama wafadhili kuepuka kutumia misaada hiyo kujinufaisha binafsi.
Katibu katika idara hiyo Caren Agengo amesema kuchapisha taarifa za kutambulisha mtoto ni kosa linaloweza kumfanya mhusika kutozwa faini ya hadi shilingi laki tano,kifungo cha hadi miezi 12 au ghadhabu zote 2.