Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Migori Zachari Okoth Obado, amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa hatia ya kumuua aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno mnamo mwaka wa 2018.
Hukumu hiyo imetolewa na jaji wa mahakama kuu ya milimani Cecilia Wairimu Githua huku akimtaja Obado kama mhusika mkuu wa mauaji hayo .
Jaji Githua amelikataa ombi la familia ya marehemu ikiyokuwa imependekeza kwamba Obado apewe kifungo cha nje.
Wakati uo huo aliyekuwa msaidizi wa Obado Micheal Oyamo, pia amehukumiwa miaka 25 gerezani huku aliyekuwa karani katika kaunti ya Migori Caspal Obiero, akihukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani.
Hukumu ya watatu hao imepatikana baada ya kupatikana na hatia ya mauaji hayo mnamo julai mwka huu.
Sharon aliuwawa akiwa na miaka 26 na mjamzito wa miezi 7.