Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mikumi, Tanzania na mwanamuziki wa nyimbo za aina ya Bongo flava Profesa Jay aonekana katika video moja inayo sambaa mitandaoni akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Kabla ya kufanyiwa upasuaji amekua akiugua kwa muda hadi kufikia sasa. Alifanyiwa upasuaji na kutatiza kuzungumza kwake huku anatumia mbinu mbadala kuzungumza na akawekewa paipu inayo msaidia kusikika na wengine.
Katika mazungumzo yaliyofanyika hapo awali mwanamuziki mkongwe huyo asema ya kwamba "Ingawa magonjwa ni mawaidha watu wanasema, lakini watu wanakufa sana, kwa mimi niliyekaa ICU siku 127, unajua kule ICU watu hali zao mbaya sana, kujikuta ICU na una survive siku 127 sio mchezo."
Alipokuwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alipata mshtuko wa moyo (Cardiac arrest) mara tatu na moyo wake uligoma kupiga kwa dakika 45 huku madaktari na matabibu walipofika na kumsaidia.