Na Elijah Muthini
Hali ya ukame unatarajiwa kutawala katika maeneo mengi kwa kipindi chote cha wiki hii (27 Januari-2 Februari 2026) hali itakayochangia kuwepo kwa hali ya hewa tulivu.
Hata hivyo, maeneo machache yanatarajiwa kushuhudia mvua nyepesi za asubuhi, hivyo wakaazi wanashauriwa kuwa makini hasa katika saa za usiku. Joto la mchana linatarajiwa kuwa la wastani hadi kufikia nyuzi joto 31–32°C, huku nyakati za usiku zikiwa na hali ya baridi kidogo kwa wastani wa nyuzi joto 25°C.
Upepo wa wastani unatarajiwa kuvuma kwa wiki nzima kwa kasi ya mita 6–10 kwa sekunde hali inayoweza kuathiri baadhi ya shughuli za nje pamoja na shughuli za baharini.
Kwa upande wa Baharini, mawimbi yanatarajiwa kuwa ya wastani yakifikia urefu wa mita 1.0 hadi 1.8. Kwa ujumla, hali ya hewa inatarajiwa kuwa nzuri, lakini wasafiri wa baharini na wavuvi wanaoelekea maeneo ya maji ya kina kirefu wanashauriwa kuchukua tahadhari zinazohitajika.
Endelea kupata taarifa sahihi za hali ya hewa, jiandae mapema na panga shughuli zako kwa busara katika wiki hii.