CHANGAMOTO ZA KUSITISHWA KWA MIRADI INAYOFADHILIWA NA USAID
Blog
Published on 18/02/2025

Kusitishwa kwa miradi iliyokuwa ikifadhiliwa na shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani la USAID  kumeathiri pakubwa baadhi ya shughuli pamoja na nafasi za ajira kwa waliokuwa wakisimamia miradi mbalimbali hapa nchini.

 

Kusitishwa kwa miradi iliyokuwa ikifadhiliwa na shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani la USAID  kumeathiri pakubwa baadhi ya shughuli pamoja na nafasi za ajira kwa waliokuwa wakisimamia miradi mbalimbali hapa nchini.

 

Sekta ya afya ni mojawapo ya sekta zilizoathirika ikizingatiwa kuwa shirika la  USAID lilifadhili programu muhimu kama vile PEPFAR dawa ambazo ni za kuzuia malaria na huduma za afya ya uzazi. 

 

Endapo mradi huo utatupiliwa mbali kabisa basi huenda ukatatiza shughuli za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi hali itakayoathiri familia zilizoathirika.

 

Aidha wanafunzi wengi nchini hasa maeneo ya mashinani,hunufaika na programu za elimu zinazoungwa mkono na USAID na kufikia sasa wanafunzi wengi wameathirika kwa kukosa ufadhili huo.

 

Mbali na hayo wafanyibiashara waliokuwa wakitegemea shirika hilo pia wameachwa njia panda,programu zinazokuza demokrasia pamoja na kuinua haki za kibinadamu bila msaada wa USAID basi huenda mashirika ya kiraia yanayotetea utawala bora yataweza kuhangaika.

 

Kufikia sasa mashirika ya ndani pamoja na serikali kwa jumla ina jukumu la kuhakikisha wanaziba pengo lililoachwa ili kuhakikisha miradi iliyoanzishwa haikomi.

 

Ikumbukwe kuwa miradi yote iliyokuwa ikifadhiliwa na shirika la USAID ilisimamishwa kwa siku 90 mnamo tarehe 20 mwezi jana baada ya rais wa Marekani kuapishwa rasmi.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online