UTABIRI WA HALI YA HEWA MOMBASA
By Dayo Radio
Published on 21/01/2026 09:22
Blog

Na Elijah Muthini 

Kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa wiki hii (20-26 Januari) hali ya ukavu unatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi, huku maeneo machache yakitarajiwa kushuhudia mvua nyepesi za asubuhi.

Joto wakati wa mchana litakuwa la wastani huku likitarajiwa kufikia kati ya nyuzi joto 31 hadi 32, huku joto la chini wakati wa usiku likitarajiwa kuwa takribani nyuzi joto 25. Upepo wa wastani unatarajiwa kuvuma katika kipindi chote cha wiki, huku upepo mkali ukitarajiwa mwanzoni mwa wiki. Kasi ya upepo inatarajiwa kuwa kati ya mita 8 hadi 12 mita kwa kila sekunde.

Hali ya bahari kwa ujumla itakuwa ya wastani hata hivyo, bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa mwishoni mwa wiki, yakifikia urefu wa kati ya mita 1.2 hadi 2.2.

 

Wananchi wameshauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari zinazofaa ili kuhakikisha usalama wiki hii.

Comments
Comment sent successfully!