AFISA MMOJA WA POLISI AFARIKI NCHINI HAITI.
By Dayo Radio
Published on 01/09/2025 15:43
News

Huduma ya Kitaifa ya Polisi nchini (NPS) imethibitisha kifo cha afisa mmoja wa polisi wa Kenya aliyekuwa akihudumu chini ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama nchini Haiti (MSS)

Afisa huyo alifariki dunia usiku wa Jumapili katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Kenscoff–Pétion-Ville, eneo la Pèlerin 9, wakati wa operesheni ya uokoaji.

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya afisa huyo pamoja na raia wawili, huku maafisa wengine wanane wa MSS wakijeruhiwa, watatu kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Kulingana na Msemaji wa Polisi, Muchiri Nyaga, ametuma salamu za rambirambi kwa familia na jamaa wa marehemu na kuahidi msaada wa NPS katika kipindi hiki kigumu.

Marehemu atasafirishwa kurejea nyumbani nchini Kenya, huku waliojeruhiwa wakiendelea kupokea matibabu hospitalini.

Comments
Comment sent successfully!