UTABIRI WA HALI YA HEWA PWANI
By Dayo Radio
Published on 17/02/2026 21:52
News

Na Elijah Muthini 

Hali ya hewa kavu inatarajiwa kuendelea katika kipindi chote cha wiki hii (17-23 Februari) huku hakuna mvua kubwa inayotarajiwa katika maeneo mengi ya ukanda wa Pwani. Joto la mchana litabaki kuwa juu na likitarajiwa kufikia kati ya nyuzi joto 32°C hadi 33°C, wakati wa usiku hali itasalia kuwa ya joto la wastani lenye nyuzi joto 25°C.

Upepo wa wastani wenye kasi ya mita 6 hadi 8 kwa kila sekunde utaendelea kuvuma, hali itakayosaidia kupunguza makali ya joto hasa katika maeneo ya Pwani na sehemu zilizo wazi. Baharini hali inatarajiwa kuwa shwari kiasi, huku urefu wa mawimbi ukitarajiwa kuwa kati ya mita 0.5 hadi 1.5. Hii ni hali nzuri kwa shughuli za baharini kama vile uvuvi, usafiri wa majini pamoja na burudani za ufuo wa bahari.

Wananchi wanashauriwa kunywa maji ya kutosha, kujikinga dhidi ya miale ya jua kali, na kuchukua tahadhari zinazofaa huku hali ya hewa tulivu na thabiti inatarajiwa katika wiki hii.

Comments
Comment sent successfully!