SERIKALI KUSHIRIKISHA TAASISI ZAKE KATIKA MAFUNZO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA SEKTA YA NGUO.
By Dayo Radio
Published on 29/08/2025 15:48
News

Serikali imeahidi kushirikisha taasisi zake zote kupokea mafunzo ya utunzaji wa mazingira katika sekta ya nguo.

Hayo ni kwa mujibu wa katibu katika wizara ya vyuo vya anuani nchini-TVET Dkt, Esther Muoria.

Akiongea mapema leo mjini Mombasa, Dkt Muoria amepongeza shirika la Edukans Kenya kwa kutoa mafunzo kwa taasisi hizo ambapo jumla ya wanafunzi 2,300 wanatazamiwa kufaidika na mafunzo hayo, baada ya walimu wao kupitia mafunzo hayo hapa Mombasa kutoka kwa shirika hilo.

"Nimepongeza shirika la Edukans Kenya kwa kutoa mafunzo kwa taasisi hizo ambapo jumla ya wanafunzi 2,300 wanatazamiwa kufaidika na mafunzo hayo, baada ya walimu wao kupitia mafunzo hayo hapa Mombasa kutoka kwa shirika hilo," alisema Dkt. Esther Muoria.

Mkurugenzi wa Edukans tawi la Kenya Mary Mugo amesema mafunzo hayo ni muhimu kuwafikia wakenya hasa vijana, kwani sekta hiyo ni ya nne kwa uchafuzi wa mazingira.

"Mafunzo haya ni muhimu kuwafikia Wakenya hasa vijana, kwani sekta hiyo ni ya nne kwa uchafuzi wa mazingira," alisema Mary Mugo, Mkurugenzi wa Edukans tawi la Kenya.

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!