SONKO ALALAMIKIA CAF KUHUSU MECHI YA HARAMBEE STARS DHIDI YA MADAGASCAR.
By Dayo Radio
Published on 25/08/2025 13:07
News

Gavana wa zamani wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko, amewasilisha malalamishi kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF, akitaka mechi ya robo fainali ya CHAN kati ya Harambee Stars na Madagascar irejelewe.

 

Sonko anadai waamuzi walionyesha upendeleo na kubatilisha mabao mawili ya Kenya bila kupitia mfumo wa VAR au kushauriana na maafisa husika wa timu. Kupitia wakili wake Arnold Oginga, Sonko anasema hatua hiyo ilinyima Kenya nafasi ya haki ya kusonga mbele.

 

Miongoni mwa suluhu anazotaka ni kufutwa kwa uamuzi wa kubatilisha mabao hayo, kufutwa kwa matokeo ya mikwaju ya penalti, na Harambee Stars kupewa ushindi. Iwapo hilo halitawezekana, anapendekeza mechi hiyo irejelewe.

 

Safari ya Harambee Stars kwenye mashindano hayo ilikatishwa usiku wa Ijumaa baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4–3 na Madagascar katika uwanja wa Moi Kasarani.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!