KWAHERI JOTA NA ANDRE.
By Dayo Radio
Published on 04/07/2025 12:42
Sports

Ulimwengu wa soka unalia, machozi kila Kona ,mojawapo ya vipaji safi zilizoshuhudiwa ullimwenguni kaondoka asirudi tena.Hakuwa tu mchezaji wa soka bali alikuwa msanii uwanjani, mpira ukiwa miguuni make alichora tabasamu kweye nyuso za mashabiki wengi.Raia wa ureno na Mshambulizi wa timu ya Liverpool Diogo Jota ameaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani huko Uhispania.

Jota amefariki akiwa na umri wa miaka 28, majuma mawili baada ya harusi yake na kuwaacha mkewe na Watoto watatu.Kulingana na taarifa kutoka nchi hiyo mchezaji huyo amefariki na nduguye ADRE SILVA waliyekuwa wameandamana naye kwenye gari lake aina ya lamb.

Ikumbukwe kuwa jota alifungua ukrasa wa ndoto yake ya kabumbu na klabu ya percos de Ferreira, kasi yake, weledi wake na ushupavu ulivutia klabu ya Athletico Madrid, baadae akajiunga na porto kwa mkopo. Wino mzito uliandika historia ya Diogo jota alipojiunga na klabu ya Wolverhampton pale baadae alisajiliwa na THE REDS na kuujaza mkataba wa miaka mitano ambapo aliwasaidia Liverpool kuishinda kombe la mabingwa uingereza . mshambulizi huyo ameupiga mwingi chini ya wakufunzi au makocha kadhaa tajika ikiwemo NUNO ESPIRITO wa PORTO wakati ule akiwa na jugen klop Pamoja na mkufunzi wake wa hivi majuzi Arne slot Ughani Anfield. Akizikwa hivi leo, wanaspoti, jamaa marafiki, taifa na mataifa wamezidi kutoa jumbe zao za rambirambi kwa familia. Makiwa kwa familia ya soka kiujumla kwa kumpoteza staa huyo. Makala ya spoti , DAyo radio na mbithi David.

Comments
Comment sent successfully!