HISTORIA KASORO SEKUNDE
By Dayo Radio
Published on 27/06/2025 14:45
Sports

 

Katika uwanja wa Stade Charléty jijini Paris, mwanariadha mashuhuri wa Kenya, Faith Kipyegon, alijitosa kwenye jaribio la kihistoria la kukimbia maili moja chini ya dakika nne, jambo ambalo halijawahi kufanywa na mwanamke yeyote duniani.

Kwa msaada wa waongoza kasi na teknolojia ya mwanga wa kasi, Nyota huyo mshindi wa Olimpiki na mbio za dunia alikimbia kwa kasi ya kushangaza na nidhamu ya hali ya juu. Alivuka mstari wa mwisho kwa muda wa dakika 4 na sekunde 6 nukta 42, hivyo kushindwa kuvunja ukuta wa dakika nne, lakini akaweka rekodi mpya ya binafsi na duniani.

Faith amesema, “Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu. Ingawa sikufikia dakika nne, najivunia nilichokifanya.”

Faith Kipyegon ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni malkia wa mbio za kati, na jaribio hili ni ushuhuda kuwa mwanamke yuko karibu kabisa kuvunja ukuta wa dakika nne.Ama kweli kipyegon aamini atarejea akiwa na nguvu zaidi na bila shaka atafanikiwa kushinda ukuta huko wa kihistoria.

Comments
Comment sent successfully!