Vijana wa ANGE POSTECOGLU ,totenham hotspur wawarindima,kuwakandamiza na hatimaye kuwabandua makinda wa REUBEN AMORIM Manchester united, huku wakijishindia kombe la Europa na kufanikisha ndoto yao ya kucheza katika kombe la mabingwa barani ulaya.TOTE walipata bao lao kupitia winga wa kulia maharufu Johnson baada ya kuwaacha mabeki hoi huku akimhangaisha mlindalango Andre onana na kuitikisa Kamba ya wapinzani.
Manchester kama vile,ARSENALI na MAN CITY sasa yamaliza msimu bila taji lolote huku mkufunzi AMORIM akiandikisha rekodi mbaya ya kuwa mkufunzi aliyepoteza mechi nyingi baina ya makocha waliokiongoza kikosi hiki cha united. Ikumbukwe kwamba united wako katika nafasi ya kumi na sita alama 38 huku wakisalia na mechi ya ASTONVILLA ligi kuu uingerezakutamatika.JE Manchester itajimudu na kurejeshea mashabiki wao raha na msisimko ughani ama mwiba utazidi kuwa huo huo. Ungana nami MBITHI DAVID tuchambue spoti kwa undaani nikikupakulia uhondo wote wa spoti ndani ya DAYO RADIO VIWANJANI.