Manchester ya mjini ama ukipenda man city watolewa donge mdomoni na vijana wa crystal palace baada ya kukung'utwa bao moja komboa ufe huku wakiikosa Kombe la FA mara ya pili mfululizo. Kinda wa wingereza na mushambulizi wa palace Zungumzia kijana Eberechi oluchi Eze alitikisa kamba mnamo dakika ya kumi na sita na kusababishia palace kushinda kombe Hilo.

Manchester city sasa wanamaliza msimu bila kombe lolote kama Arsenali walibanduliwa kwenye mashindano ya kombe la mabingwa barani ulaya na vigogo wa Paris zungumzia PSG. Je wawili hawa watajilusanya na kuwika msimu ujao? Ungana na kikosi kizima cha Dayo radio viwanjani utupee maoni yako, ni kipi haswa timu izi mbili zinafaa kuzingatia na kurejesha ukali wao?