Reggae Legend Cocoa Tea Amefariki Dunia
Music
Published on 12/03/2025 by Dayo Radio

Mkongwe wa muziki wa Reggae, Colvin 'Cocoa Tea' Scott, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65. Kifo chake kimethibitishwa na mkewe, akieleza kuwa mwimbaji huyo mashuhuri alifariki kutokana na shambulio la moyo (cardiac arrest).Cocoa Tea alikuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa Reggae, akifahamika kwa nyimbo maarufu kama Rikers Island, Young Lover, Tune In na Barack Obama. Ujumbe wake wa amani, mapenzi na haki za kijamii kupitia muziki wake ulimfanya apendwe na mashabiki wa Reggae duniani kote.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zinaendelea kufuatiliwa. Pumzika kwa amani, Cocoa Tea.

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online