Jamii ya wagonjwa wa kifafa kutoka kata ndogo ya Kadzandani eneo bunge la Nyali waliandaa mandaamano ya amani kama ishara ya maadhimisho.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Simon kakawa, wagonjwa hao waliandaa msafara wa kuelimisha na kushinikiza jamii kuhusu changamoto wanazopitia.
"Mimi kama msimamizi wa wagonjwa wa kifafa tunapitia sana changamoto nyingi na ningependa kuisihi serikali ya kaunti ya Mombasa kuja na mbinu itakayotusaidia ili tupate madawa badala ya kwenda mpaka kaunti ya Kilifi"
Ni kauli iliyoungwa mkono na mmoja wa wazazi wa watoto wenye ugonjwa huo akitaka serikali za kaunti na serikali kuu kuwapa kipao mbele hususani wanapo tafuta huduma Muhimu za serikali.
"Mgonjwa wa kifafa anafaa kupewa kipaumbele katika na kuhakikisha anapata huduma muhimu kama wengine swala la kuwatenga sio jambo nzuri."
NA HARRISON KAZUNGU.