Kipute cha Dola Super Cup Mombasa chafika tamati uga wa Mwahima Likoni,timu mbili Likoni One dhidi ya Likoni Two walimaliza dakika tisaini wakiwa nguvu sawa 1 - 1,jambo ambalo lilimlazimu muamuzi wa Kati mwenye tajriba ya juu bwana Hussein kupeleka kesi hiyo mahakama ya matuta ya penalti.
Likoni One walifaulu kutawazwa mabingwa wa Mombasa kwa tofauti ya mikwaju 6 - 5.
Viongozi kadhaa wa serikali ya kaunti ya Mombasa walikuepo wakiongozwa na gavana Abdulswamad Sharrif Nassir.Vilevile mbunge wa eneo hilo Mh.Mishi Mboko alimrai gavana kufanya ukarabati uwanja huo ili kufikia viwango vinavyokubalika kimichezo,kwa upande wake gavana alikubali ombi hilo na kukariri mwezi ujao wa agosti ukarabati utaanza mara Moja.Katika baadhi ya zawadi gavana aliwaongezea timu zote mbili laki moja kama hongera ya mchezo mzuri wenye nidhamu,vile vile alishukuru kampuni ya unga Kitui Flour Mills kwa kazi nzuri wanayofanya kuinua vipaji kanda ya pwani.
By: Fadhili Mzee