KEN ODHIAMBO ASAINI MKATABA NA BANDARI FOOTBALL CLUB
Sports
Published on 18/07/2024

Naibu Kocha mkuu wa timu ya taifa Harambee Stars Ken Odhiambo, ametia saini mkataba wa kujiunga na klabu ya Bandari Football Club mapema hii Leo.

Mkufunzi huyo amechukua hatamu kutoka kwa aliyekua kocha msimu 24/25 John Baraza.

Katika Mpangilio mpya Kocha Baraza atakua naibu mkufunzi,huku Jerry Onyango akitarajiwa kuendeleza majukumu yake ya ukufunzi wa makipa.

Kwenye mahojiano ya kipekee na mkurugenzi mkuu wa Bandari football club Tony Kibwana ameahidi kuwa  bodi itampa usaidizi wa kila aina Odhiambo ilikuziba mapengo yaliowachwa na wachezaji waliohama baada mikataba yao kuisha.

By: Fadhili Mzee

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online