POLISI MTWAPA WAKAMATA WASHUKIWA SITA KWA TUHUMA ZA WIZI
By Dayo Radio
Published on 25/10/2026 14:38
News

Polisi mjini Mtwapa, kaunti ya Kilifi, wamewakamata washukiwa sita na kufanikiwa kunasa bidhaa mbalimbali zinazoshukiwa kuwa za wizi, akiwemo mbuzi, pamoja na misokoto ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa ripoti za polisi, washukiwa watano walikamatwa jana katika operesheni iliyoongozwa na taarifa za kijasusi katika eneo la Kipapuro, huku mshukiwa wa sita, Said Abdi Rashid, akikamatwa katika nyumba iliyokuwa imetambuliwa akiwa na bidhaa alizoshindwa kuthibitisha umiliki wake.

Washukiwa hao wanatarajiwa kusaidia polisi katika uchunguzi zaidi kuhusu bidhaa zilizopatikana na tuhuma zinazowakabili.

Comments
Comment sent successfully!