BUNGE LAWEKA MIKAKATI YA KUKAMILISHA KAZI KABLA YA UCHAGUZI WA 2027.
By Dayo Radio
Published on 08/09/2026 20:19
News

Kamati ya uhusiano ya Bunge la Kitaifa imeandaa kongamano la kimkakati mjini Mombasa, likilenga kutathmini utendaji, uwajibikaji na ufanisi wa kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake ya kibunge.

Kongamano hilo pia linatoa fursa kwa viongozi na wadau mbalimbali kujadili masuala yanayohusu uendeshaji wa shughuli za Bunge, maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 pamoja na mapendekezo ya mabadiliko ya baadhi ya vipengee vya kisheria vinavyohusiana na shughuli za Bunge.

Kongamano hilo linalenga pia kuweka mikakati ya kuhakikisha Bunge linakamilisha shughuli zake muhimu kabla ya nchi kuingia katika kipindi cha uchaguzi, huku likizingatia wajibu wake wa kikatiba katika kusimamia matumizi ya rasilimali za umma na kuhakikisha Serikali inawajibika kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mombasa, Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa, Gladys Boss Sholei, amesema Bunge limeweka mikakati ymaalum ya kuhakikisha kazi muhimu za kibunge zinakamilishwa kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Kwa upande mwingine, maandalizi ya uchaguzi yanatarajiwa kuleta mabadiliko katika shughuli za kisiasa na kitaifa, hivyo Bunge linataka kuhakikisha kazi zake muhimu hazikwami kutokana na mchakato huo.

Hata hivyo ametaja kuwa kuweka mikakati ya mapema, Bunge linalenga kukamilisha miswada, ripoti za kamati na uchunguzi wa matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha masuala muhimu yanayohitaji maamuzi ya kibunge yanashughulikiwa kwa wakati.

 

Kulingana naye Kongamano hilo ni sehemu ya juhudi za Bunge kuimarisha utendaji na uwajibikaji wa kamati zake, huku likijiandaa kwa kipindi muhimu cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

 

Hata hivyo Viongozi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kuendelea kuwa taasisi inayowajibika kwa wananchi na kuhakikisha majukumu yake ya kutunga sheria, kuisimamia Serikali na kuwakilisha maslahi ya wananchi yanaendelea kutekelezwa kwa ufanisi.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!