Kwa taarifa, huduma za macho, masikio na ya kutosikia katika eneo la Pwani zimepata msukumo mpya baada ya kuzinduliwa rasmi kwa miradi miwili inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika leo, Jumatatu tarehe 21 Septemba 2026 mjini Mombasa ukitanisha washirika wa maendeleo, wawakilishi wa serikali, wataalamu wa afya pamoja na wadau wa jamii.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mgeni rasmi Dkt. Barba Qureshi amepongeza uzinduzi wa miradi hiyo, akisema ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya ya macho, masikio na halibya kutosikia katika eneo la Pwani.

“Uwekezaji katika huduma za macho, masikio na hali ya ktosikia ni muhimu kwa sababu changamoto za kuona na kusikia zinaweza kuathiri elimu, ajira, mawasiliano na maisha ya kila siku ya wananchi,” amesema Dkt. Barba Qureshi.
Dkt. Qureshi amesema changamoto hizo zinahitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali, wataalamu wa afya, washirika wa maendeleo na jamii ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi wengi zaidi, hususan wale wanaokabiliwa na changamoto ya kupata huduma maalumu za afya.
“Tunapaswa kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha wananchi wanapata uchunguzi na matibabu kwa wakati, kwa sababu uchunguzi wa mapema unaweza kusaidia kubaini matatizo ya macho na usikivu kabla hayajawa makubwa,” amesema.

Aidha, Dkt. Qureshi amesisitiza umuhimu wa kuongeza uelewa miongoni mwa wananchi kuhusu uchunguzi wa mara kwa mara wa macho, masikio na usikivu, akisema hatua hiyo inaweza kusaidia kubaini changamoto za kiafya mapema na kuwawezesha wananchi kupata matibabu kwa wakati.
Amesema uzinduzi wa miradi hiyo unaonyesha dhamira ya wadau mbalimbali ya kushirikiana katika kuboresha huduma za afya na kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi katika eneo la Pwani.
Hafla hiyo imehitimishwa kwa shughuli mbalimbali za kuashiria uzinduzi rasmi wa miradi hiyo, huku wadau wakieleza matumaini kuwa mipango hiyo itachangia kuongeza upatikanaji wa huduma bora za macho, masikio na usikivu katika kaunti za Pwani.
NA HARRISON KAZUNGU